JIFUNZE ZAIDI KUHUSU WACHAGGA
Vikundi vya Wachagga [ hariri | hariri chanzo ] Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa ki jiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki ( Tarakea , Rombo ) hadi magharibi kwa Kilimanjaro ( Siha , Machame ). Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo , Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndio inajulikana na wengi kama Kirua Vunjo. Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kama Wa-Mwika, Wa-Mamba , Wa-Marangu , Wa-Kilema ,na Wakirua.Makabila mengine ni Wa-Old Moshi , Wa-Kibosho , na Wa-Machame , Wa-Uru , na Wa-Siha . Lugha ya Kichagga [ hariri | hariri chanzo ] Lugha ya Kichagga inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa...